To listen audio of the debate, click the play button
A critique by Kiranga
The exchanges start on a civil enough tone, and goes on to even jovial at times. This is a relief in so far as we have witnessed some less than civil exchanges, especially at the grassroot level. I have always advocated a competitive democracy that remains civil. The Jamaicans are having a lot of problems with their politics, with the JLP and PNP constantly causing political eruptions on the streets of Kingston and elsewhere on that island. I would not want to see the Tanzanian scenario degenerating into that.
Prof. Baregu kicks off with the question of education. Sadly, for a person of the professor’s caliber, I would expect some solid statistics. I did not hear any on this front. I know Mr. Kinana later produced an anecdote to demonstrate the Kikwete administration’s commitment to education, raising the number of students in higher learning institutions from a paltry 38,000 to around 120,000.This is impressive, and while I do not wish to sound unappreciative on this commendable feat, my concerns remains with the quality of the education provided. Elsewhere I saw the First Lady giving a rather detailed, if not exactly spirited, speech centred on eductaion while campaigning for Shukuru Kawambwa in Bagamoyo, it was also impressive.I have to say if you go by the sheer numbers reported, it is hard to say Kikwete has done nothing on the education front (and I am not a Kikwete fan by any stretch, so this is not some lovefest). Maybe he could have done better and Prof. Baregu is attempting to show that CHADEMA can do better, but without specifics this comes off hardly convincing.
CHADEMA’s policy of free education for all ( or at least non-need based full grants) is hardly practical, highly uneconomic and mostly an unfair attempt at statist largesse. Even a die hard advocate for free education like Mwl. Nyerere, a person whose gravita CHADEMA uses constantly to tout their legitimacy, denounced the cause as foolhardy. In his May Day 1995 speech in Mbeya Nyerere argued that Tanzania now has millionaires who can afford to pay for their children’s education, so they should pay. I totally understand that there are some people who need help, and while I do not advocate governmental largesse and the welfare state, I do understand that we are not at a stage where the government can totally withdraw from some social services. I get that. But why do we need to have a non-need based grant system beats me. This means a millionaire’s son has the same access to these grants as does a peasant’s son from Malampaka ? Where is the fairness here? In Switzerland even the penalty of a traffic offence is determined by a person’s wealth, because they figure if you have a flat fine, some people (especially millionaires) would view a $ 100 fine as pocket change and not worth worrying over. I am not saying we should adopt a proportionate payment system, but at least make everybody pay what they can afford, don’t give out unmitigated stipends and full unequivocal grants. Especially if our resources are meagre and must be used very frugally in the first place.
I agree with Baregu’s/ CHADEMA’S vision of introducing more elective offices and doing away with presidential appointees as DC’s and RC’s for example. This is in tune with my vision of changing the topography of our politics, changing the structure of power from a top down, appointment based system which is more accountable to the president and prone to political clientilism and temptations of presidential largesse, to a bottom up, people centred, merit based and more people accountable leadership.
On CCM’s candidates passing unopposed, this clearly shows the opposition’s weakness and validates CCM’s claim that the opposition is made up mainly of “election parties”. The rebuttal from Prof. Baregu is hardly fitting. The number of constituencies with no opposition candidates is so high and does not match the number of constituents with claimed irregularities. Claims of opposition candidates being bought off just goes to show Tanzanians that the opposition is not serious enough to nominate serious candidate. If a party can nominate someone who can easily be bought, I don’t have confidence with that party’s maturity and vetting process.
The truth remains many of the opposition candidates are very weak, unfamiliar with the issues, unexposed and even naïve. While I cannot say that CCM does not have the same problem for sure, I would expect the opposition to give Tanzanians a better choice, otherwise what is the point of replacing one mediocrity with another ? Especially if the present mediocrity is at least known (zimwi likujualo halikuli likakwisha). The CHADEMA Kilombero constituency candidate is on record saying one does not need anything special to be MP. CHADEMA readily takes CCM rejects, with ceremonious publicity, no vetting or indoctrination. This leaves people wondering, are the CCM rejects the best that CHADEMA can offer ? What if CCM is planting it’s intelligence into CHADEMA? There is actually a case (I believe in one of the Tabora constituencies) where a CCM reject was given the CHADEMA nomination, only not to return the forms and cause the CCM candidate to go unopposed. What if this candidate had decided to contest, win under the CHADEMA banner, and sabotage the CHADEMA agenda within the parliament ?
The notion of MP’s passing unopposed is actually unconstitutional. Clause 66 of the constitution clearly list the types of MPs and how they get to be MPs. Nothing is mentioned on unopposed MPs sailing to parliament without actually being elected by Tanzanians ( not only CCM members in CCM primaries). I am surprised the opposition doesn’t mention this, maybe it is a shameful issue that they did not field a candidate in the first place and therefore mentioning that would be adding insult to injury. But I would like to see the people getting even a “YES/ NO” vote, if only to give the MP legitimacy as chances are it would be very hard to lose in an unopposed election. Overall, this is symptomatic of a weak opposition. There is a n article from “The Citizen” detailing the demise of competitive democracy and the opposition in Tanzania (click).
On voter registration card manipulation, CHADEMA should come with a more credible story, even set up a trap to build a concrete case.
Then the spin and fluff kicks in full blown mode with Kinana asking Baregu to apologize for something he did not say. Kinana gives some sound, if general, unsolicited and self serving, advice on the need for CHADEMA to build it’s clout. This is a genuine issue. And while CHADEMA claims that it is a young party, 18 years is not so young and if this was a person, CHADEMA would be of voting age now. Kinana also mentions the issue of CCM rejects being celebrated at CHADEMA. I pointed this out earlier elsewhere as an issue. And while I do not outright oppose party switching, I would want at least a vetting and indoctrination period.
Professor Baregu rightly rejects the categorization of his misconstrued comments as a snob to Tanzanians. He went on to invoke the Nyalali Commitee’s findings and recommendation on building a more democratic environment -a tired, if valid- excuse. What the professor does not say is how has CHADEMA pressured the government and rallied it’s base to have these recommendations actually instituted. Prof. Baregu talks about the quality of the opposition input in the parliament as endorsed by the speaker, and how this input is undermined by the sheer number of CCM MPs. Perhaps Prof. Baregu is milking the speaker’s graceful and diplomatic coalition building comments a bit too far, perhaps not. But as he further points on, without a majority the opposition will remain ornamental.
On negative campaigning, Kinana accuses CHADEMA of being over litigious and serial complainers, hence undermining their own credibility. While CCM is good at politicking and framing the CHADEMA narrative to CCM’s advantage, and regardless of the merit of CHADEMA’s claims, there are already reports of certain sects of the workers movements announcing it’s alienation from Slaa/ CHADEMA in what is perceived as Slaa’s move to block their chances. This then becomes a question of principles over political expediency, and I am always for principles. CHADEMA should stand it’s grounds where it thinks elections regulation are violated. CCM cannot be objective in judging CHADEMA as over litigious, that is what we expect to hear from them. While I would like to see a democracy that runs smoothly without the interference of the courts and NEC, when necessary, the appeal systems should be used with no fear of appearing ‘over litigious’. Let the people decide whether CHADEMA is over litigious, perhaps our opposition has been “under litigious” all along and it needs to step up it’s game in that aspect.
On the question of a “level playing field” Prof. Baregu fails to make a coherent case. State media news outlet just started giving a fair share of airtime to opposition parties after some vehement protests, I expected Prof. Baregu to voice his chagrin on this, instead he downplayed the whole issue as of a minor importance and chose to dwell on the CCM stadiums -which rightly belong to all Tanzanians- being used as CCM’s properties, a matter which shouldn’t have to wait until election time to be adressed. This further validate Kinana’s claims that the opposition parties are election parties, how has the opposition raised this as an issue before ? Was it ever brought up and pursued in parliament? If it was I did not hear it, and not from lack of following.
Prof. Baregu went on to talk about the sad cowardice acts of CCM censoring it’s candidates. This is pure and simple censorship, however spinned. It looks like either CCM doesn’t have much of a record to defend, or is not very confident of it’s candidates ability to champion that record, possibly even both. A prominent up and coming CCM cadre was quoted as endorsing this move as “ good politics” meaning politics in the negative sense of obfuscation and Machiavellian manipulations. According to him the country is poor, CCM does not have much to show for all it’s years in power, a lot of the promises made in 2005 are still unrealized, so it makes sense to refrain from debates. And this guy is one of the rising stars.To him political expediency comes prior to accountability to the people and transparency. If this learned star has this mindset I shudder to think what the number of semi-literate candidates will think. They are probably breathing a sigh of relief and thanking the party bigwigs for not exposing their incompetency. This is not a good look for CCM at all. And all the obfuscation Kinana gave, about the president and CCM candidates needing to go to the people are so transparent, I can see clearly through them. Is CCM this much anti-press, anti-intellectuals and anti-transparency ? What does it fear? Kinana couldn’t answer this on the issues and resorted to obfuscation and fluff.
Baregu claims the demographics of Tanzanian voters has changed so much, and the current body of voters is very youthful, and he expects his candidate to win confidently (no mention of possible results altering vote machinations was made). This remains to be seen.
Mimi sikufurahishwa na kauli za Kinana mwishoni kabisa aliposema Slaa sio saizi ya Kikwete… Ilikuwa below-the-belt blow, na sikutegemea ile kauli kutoka kwake.
Nashukuru mwandishi ametuonesha maana ya mdahalo. Kwasababu wakati nausikiliza mara ya kwanza nilidhani Beregu kajitahidi kuhoji vitu vya msingi. Ila nimetoka kuusikiliza tena na kufikiria kwa makini, kweli kambi ya upinzani itabidi wajipange. Yaani Kinana hakutetereka.
Sasa, tungekuwa na midahalo kama hii hadi kwa wagombea wa Urais nadhani tungejifunza mengi zaidi ya tuliyosikia kwenye huu mjadala wa Beregu na Kinana.
Ingawa nami sikubaliani au sijafurahishwa na “maendeleo” yaliyoletwa na CCM, kambi ya upinzani bado haijanishawishi kama wana uwezo wa kuongoza Serikali — badala ya kutumia muda vizuri, kila baada ya Uchaguzi kukaa chini na kujipanga, watu wa Upinzani huonesha mwamko wakati wa kampeni tu. Hii sidhani kama italeta mabadiliko ambayo wengi tunayalilia.
Ujue unategemea kama chama kina zaidi ya miaka 15 kingeweza kuwa na nguvu, lakini bado CHADEMA wanasuasua. Kuna mengi ya kujifunza kutoka kwa CUF Zenji!
it’s a wonderful listen, jamaa wa BBC aliyewahoji ni mtanzania au mkenya?
@ Mgumu, na mimi niliona hilo ndiyo maana nikasema Kinana akaingia kwenye obfuscation and fluff hapo. CCM ni chama kinachojivunia kuthamini utu wa watu wote bila matabaka, sasa haya mambo ya kusema Mtanzania fulani si “size” ya mwingine sio tu hayana ile humility inayodaiwa na CCM, bali pia yanaonyesha kiburi fulani ambacho si kizuri kwa watu wanaoomba kura. Muomba kura anatakiwa kusema “mpinzani wangu mzuri, lakini mimi mzuri zaidi”. Kila mtu ana uzuri na ubovu wake.Kusema fulani si saizi yetu ni dharau na hakuonyeshi busara wala usomi, ni kama lugha za mipasho zaidi kuliko siasa za kitaifa.
@ kigogo Sina hakika ila alijitahidi. Ingekuwa bora zaidi kama kungekuwa na mkutano wa hadhara halafu Kinana na Kikwete on one side na Slaa na Baregu upande mwingine (au hata na wagombea wengine) wangeweza kuulizwa moja kwa moja.
Kazi ipo…..CCM wanaweza sana kujitetea…
Afu jamani huu upinzani hata mie siuelewi…..unawekeza sana ktk kipindi cha kampeni tu, siku nyingine kimyaaaaaaaaa ndio wanaongea bungeni mfano Dr Slaa lakini mi naona nt enough…hii spirit waliyonayo sasa katika kampeni uwa inaenda wapi after kampeni jamani????
Na sera ya CHADEMA katika elimu kwangu ni kauli ya kufikirika…….naamini ni ndoto za alinacha hizo!
Ni maoni yangu tu jamani…….
Kweli kazi ipo.
Kwanza ningependa kusema yafuatayo: Mwandishi amejitahidi kuchambua mjadala vizuri, kwa kujadili yale yaliyojadiliwa na Beregu na Kinana. Heko kwa hilo.
Ingawa nasita kutumia huu mdahalo ku-generalize mwelekeo wa kambi ya upinzani, nashindwa kujizuia kufanya hivyo. Cha kushangaza hata Jenerali Ulimwengu naye alishaandika makala kuhusu hali ya kambi ya upinzani nchini (kwamba hawafanyi kazi wanayopaswa kufanya), lakini hakuna aliyeng’ang’ania au kusema Jenerali ni mwana-CCM! Kwasababu yeye ni Jenerali, ana bifu na CCM, alivuliwa uraia n.k!
Sioni tofauti kubwa kati ya makala hii na ile ya Jenerali kusema ukweli; kwasababu zote zimegusia suala la kambi ya upinzani kucheza makida na kutokuwa makini!
Kama mpenda demokrasia, ningependa kuona midahalo kama hii ikitumiwa ipasavyo — kujadili sera na ilani za vyama na wagombea. Lakini hii makala inatusaidia kutuonesha labda Watanzania bado tuna safari ndefu hadi kufika kwenye ile policy-based politics. Ni ushabiki tu na kuanza kuitana wewe CHADEMA, wewe CCM. Maana yake, utakachosema hata kama kina mantiki ya maana, hakuna mtu wa upande wa pili atakayekaa chini na kusikiliza unachosema na kujaribu kukuelewa, kisha kupangua HOJA zako.
Sasa najiuliza, hivi, hata JK akikubali kufanya mdahalo, Watanzania tutaweza kuunyambua kwa kubadilishana mawazo juu ya mambo watakayojadili? Kama jibu ni hapana, basi nadhani ni upuuzi hata kuendelea kupiga kampeni kumshawishi JK aingie kwenye mdahalo!
Kwa kumalizia tu, kuna makala nyingine hapa ambayo inachambua ilani za wagombea urais — JK, Slaa na Lipumba [bofya].
Labda uvivu wetu – linapokuja suala la kufuatilia, kuchambua mambo/sera na kuwabana wagombea – ndio unawapa mwanya wanasiasa wengi kuendelea kufanya wanachofanya.
Mh Kiranga na mwenzio mnaoamini elimu ya BURE haiwezekani,
Naomba na mimi nitoe wazo.
Kwanza nilivyowaelewa CHADEMA, elimu itakayotolewa bure ni CHEKECHEA hadi KIDATO CHA SITA.
Kwa kuwa umemshangaa Prof. kutotumia takwimu, angalia hizi za secondary kwanza maana shule ya msingi kwa sasa ni bure.
Takwimu za Wizara ya Elimu kwa mwaka 2008 ziko hivi: Total enrolment (Form I – Form IV) was 1,222,403 (http://moe.go.tz/statistics.html). Note: This is the sum of students enrolled in Government and Non-Government Secondary Schools (i.e. shule za sekondari zote Tanzania nzima, za serekali na zile zisizo za serikali)
Assuming that enrolment rate doubles each year (which has never been recorded, kwa takwimu hizo hizo za wizara zinavyoonyesha kuanzia mwaka 2004 – 2008): Mwaka 2009 utakuwa na wanafunzi 2,444,806 na 2010 utakuwa na wanafunzi 4,889,612.
Chukua wanafunzi wote wanalipa ada ya kitado cha tano ambayo ni TShs 75,000/= kwa mwaka. Kwa mwaka 2009 serekali inahitaji TShs 183,360,450,000/= ili watoto wasilipe ada na 2010 inahitaji TShs 366,720,900,000/=. NAOMBA NIKUKUMBUSHE TENA HII NI KWA WANAFUNZI WOTE WA SEKONDARI (PRIVATE NA GOVERNMENT).
Serikali makini itashindwa ku raise kiwango hiki cha pesa ili iwatoe ujinga watu wake ikizingatiwa kuwa elimu ndio msingi wa kila kitu kihusucho maendeleo ya mtu binafsi na serikali kwa jumla!!
Sitaki kugusia pesa zinazotuka kununua mashangingi, EPA, Richmond, …… piga hesabu mwenyewe.
Elimu ya chuo kikuu tatizo liko kwenye bodi ya mikopo. Mfano: mwanaume unatakiwa upate Division ONE na mwanamke kuanzia Division TWO ili ukopeshwe. Ni wanaume wangapi wanosoma shule za kata wana jeuri ya kupiga one ili wakopeshwe? Kabla hata ya kuingia kwenye hiyo means test!! Soma kipengele cha 3.5: ELIGIBILITY FOR LOANS FOR 2010/2011 ACADEMIC YEAR (http://heslb.go.tz). Two yenyewe ni issue kwenye shule za walalahoi!!
mimi na wish tu, mdahalo ungekuwa mrefu zaidi, na ungekuwa kwenye specifics zaidi, tujue maswala kiundani. Lakini nimefurahia kuwa walifanya huo mdahalo. Naona CCM waliamua kututuliza na hii ya Kinana ili kesho waseme, si tuliwapa mdahalo, si ule wa Baregu na Kinana, CCM wasanii..mambo mengine bwana, yaani mtu mzima unapojaribu mdanganya mtoto alafu uwongo wenyewe ni wa wazi, nadhani hapo mkubwa anakuwa amejipunguzia heshima…lakini hivyo hivyo tena, tutafika, kwani si sis wote kuna kipindi tulidanganywa kuwa watoto wanapatikana baharini na kuamini, huku wengine mpaka hii leo na ndevu zao, wanaamini kuwa Santa Claus yupo kiukweli ukweli…..ndio maisha hayo I guess….
@ Mokolo
Naona hujanielewa. Nafikiri nimefanya kazi nzuri kueleza wazi kwamba sipingi serikali kutoa msaada kwa watu wanaohitaji msaada huu. Nimeelezea kwa undani kwamba nchi yetu ina watu wengi wasio na uwezo, na hawa serikali yoyote inaweza kuwajibika kuwasaidia. Nisichotaka ni hii habari ya kusema elimu bure kwa wote, ambayo itampa mtu aliyepiga bingo ya EPA ya mamilioni kadhaa ya dola za kimarekani na mkulima wa jembe la mkono ambaye nyumba yake nzima inaingiza USD 250 kwa mwaka, hawa wote wawe na uwezo wa kupata elimu bure kweli sawa hili? Katika nchi ambayo inajulikana kutokuwa na fedha ?
Progress resistant societies are centred in paternalism, while progress prone societies are centred in innovation. Our resources are meagre and in much demand, let’s recognize that.
kaka naomba tuongelee ELIMU tuu. Plz baki kwenye ELIMU YA BURE.
Kuna watoto wawili hapa uliowataja:
1. Mtoto wa Mr X ambaye wazazi wake ni waaalee waliopiga bingo ya EPA (i.e. wana pesa)
2. Mtoto wa mkulima/mfugaji wa jembe la mkono (mlalahoi)
Kati ya hawa watoto wawili yupi adhiibiwe kupata/kukosa elimu kwa sababu ya kipato cha mzazi wake? Hata kama mzazi aliiba, je hiyo inatosha kummpa/kumnyima mtoto elimu?
Je unafikiri vigezo vinavyotumika kumpa au kumnyima elimu mtoto kwa vigezo vya mzazi anazo au hana pesa vina mantiki na vinazingatiwa?
Je tukiwapa hawa watoto wote elimu ya bure bila ya kuangalia uwezo wa wazazi wao, itakuwa ni faida au hasara kwa taifa? Namaanisha ELIMU ya BURE kwa watoto wote.
@ Mokolo,
Tuseme tuna nafasi moja ili kutolea mkazo na kulielewa vizuri suala la “limited resources”
Mtoto wa mkulima hawezi kwenda Feza Academy, Kenya, Afrika ya Kusini, Uingereza wala Marekani kusoma.Kwa hiyo kimsingi akikosa nafasi hii anarudi kulima, anakosa elimu.
Mtoto wa Mr. X mwenye uwezo, hata akikosa nafasi hii ya elimu ya bure ana nafasi ya kwenda kokote kutafuta elimu, na kukosa nafasi ya kusoma bure hakutamuathiri sana.
Ndiyo maana nasema nafasi hii ya bure apewe mtoto wa mkulima ambaye hana uwezo, na kama tunataka kumpa mtoto wa Mr. X mwenye uwezo, Mr. X alipishwe ada ili ada hii ama itumike kumsomesha mtoto mwingine wa mkulima asiyejiweza, au itumike katika huduma nyingine za kijamii. Hata huyo Karl Marx aliyetetea mifumo ya serikali kuchukua majukumu ya huduma za jamii alisema “From each according to his ability, to each according to his need”. Hata Mwalimu Nyerere ambaye alikuwa ni bingwa wa kutetea elimu ya bure kwa wote mwishoni alikubali kwamba serikali maskini kutaka kumlipia kila mtu katika mtindo wa “mtego uwanasao waliokusudiwa na wasiokusudiwa” halikuwa jambo la busara, kwa maana ya kwamba wenye uwezo wa kujilipia na wajilipie.
Tunapenda kuamini kwamba “elimu bora kwa wote” italeta huduma sawa kwa wote kwenye elimu, lakini mimi naona itawanyima maskini zaidi ya itakavyowanyima matajiri.
Msikilize Mwalimu Nyerere dakika ya 4:40
http://www.youtube.com/watch?v=XvVtJGCw8T4&feature=player_embedded#!
Umenimaliza na hiyo youtube clip. Sijui ulijua mi kipenzi cha Mwl Nyerere!!
Remain blessed.
Anayestaajabu ya Mussa ataona ya Farao! Inawezekana endapo tu matumizi yasiyokuwa ya lazima kwa serikali na misamaha ya kodi isiyokuwa na tija kwa wananchi itaondoshwa. Nchi hii ni tajiri sana ila rasilimali zake haziwafaidishi walengwa bali tabaka dogo la wajanja wachache waliopo katika nafasi za kufanya maamuzi. ‘Ulimwengu, na sasa Tanzania, ina rasilimali tosha kukidhi haja ya watu waliopo. Sera mbovu na usimamizi legelege wa kuoneana haya ndo umetufikisha hapa tulipo’. Hakuna umasikini mbaya kama ule wa kuwa na hofu ya kukabiliana na mabadiliko. Usipoleta mabadiliko wewe leo kwa hiari, ‘nature’ itakulazimisha kufanya hivyo tena kwa maumivu makali.
Hofu ninayoongea ni ile ya kuwa kuwadi wa kufagilia hata mambo yanayoonekana kwa macho ya nyama. Kijana mwenye nguvu, tegemeo la taifa na jamii unahofia hata kuandika jina lako halisi kwa kuwa tu una matarajio fulani ya kubebwa na chama fulani. Ndugu yangu, unafiki huu si suluhisho la matatizo ya nchi hii bali ni koleo au jembe la kujifukia mwenyewe. Amka sasa, usiogope, kemea uovu unaoendelea na uchukue hatua thabiti na halali kulikomboa taifa hili dhidi ya wajanja wachache wanaojiona kuwa wana uchungu sana na taifa hili japo tumewapa ridhaa ya kutuongoza kwa nusu karne sasa.
Usitegemee miujiza sasa wakati huko nyuma hawakuwa na ‘substantive’ impact kwa masikini wengi. Kura yako ndo ukombozi wako. Inapokuja suala la maslahi na mustakabali wa nchi yetu, sote tuna dhamana ya kuchukua hatua madhubuti badala ya kuendekeza propaganda na ushabiki wa vyama. Hivi, Mtazania wa leo anaweza kusimama kifua mbele na kukiri kwa kinywa chake kuwa anaona fahari kuwa kwa takriban miaka 5 iliyopita, ukiacha walau ile ya Ben Mkapa kuwa1, 2, 3……… kimetekelezeka?
Maji Dar ni mfupa ulomshinda fisi japo tunazungukwa na mito kila pande. Msongamano wa magari ni sehemu ya fahari ya mji. Makazi yasiyopimwa ndo ‘landmark’. Bado unasema maisha bora yanawezekana. Mi ni wa chama hicho lakini inapokuja suala la kuzunguka vijijini na kuona jinsi watu wanavyoishi maisha ya zana za kati za mawe katika ulimwengu huu wa sayansi na teknolojia ninaumia sana. Ninaamini kuwa siku watu wakiuona ukweli katika mwanga bora zaidi basi itakuwa ndo ‘take off’ yetu kuelekea kwenye maisha bora halisi na si yale ya kinadharia.
Tunajifunza kwa kule ambako upinzani umefanikiwa kukamata walau jimbo, serikali imetekeleza ilani kwa vitendo ili kuwadhoofisha na kurudisha imani yao tena kwa wananchi.Hiyo ndo demokrasia ya kweli na ushindani maridhawa kwa mustakhabali wa nchi hii. Kuna kujisahau inabidi watu washituliwe ili waamke kutoka kwenye usingizi wa ‘kama ilivyokuwa mwanzo, sasa na hata kiama’.
Ninaamini katika ushindani unaoleta mabadiliko na si maigizo majukwaani.