One The Incredible

Ni hulka ya watu kwenye jamii kutofautiana mawazo, itikadi, mienendo na vitu vingine lukuki. Ila kuna yale ambayo wengi wetu tunakubaliana kwa pamoja; yaani, ingawa mitazamo ni tofauti, bado kuna mambo fulani yakitokea sote — au wengi wetu — tunakubaliana.

Bahati mbaya au nzuri, mambo haya hutokea kwa nadra. Lakini yakitokea, basi tunapata fursa ya kujifunza kitu fulani kuhusu jamii au kikundi cha watu husika.

Nitakupa mfano mdogo: wavulana huvutiwa na vitu mbalimbali tofauti pale wanapoona walimbwende. Lakini, ipo siku binti mmoja atapita kijiweni na “karibia” vijana wote watakubaliana kuwa ‘demu yule ni soo.’  Hata akiwa na kasoro mbili tatu.

Sizungumzii siasa (makala za siasa zitafuata baadae kidogo), na napinga kabisa tabia ya vijana kufuata mkumbo!

Fid Q alishawahi kugusia tatizo la DJs kutojua fani ya muziki alipohojiwa na Bongo Celebrity kitambo kidogo. Linalomuuma yeye binafsi na mashabiki wengi ni nyimbo za Hip Hop kutochezwa kwenye vituo vingi vya redio. Ukiuliza watu wengine, watasema hata aina nyingine za nyimbo wanazozipenda hazipigwi.

Mi’ ni mshabiki wa Hip Hop. Nukta.

Ila nakumbuka wimbo mmoja wa Mr Nice, ‘kuku kapanda baiskeli’. Sikuupenda kabisa kutokana na upuuzi uliomo mule, lakini DJs waliushikilia bango hadi kuna siku nikajikuta nauimba!

Sasa, kuna kitu kingine kimetokea Bongo. Kuna kijana anaitwa One — ni mshairi (wa kitaa) mzuri sana na anaghani kwa ufasaha wa hali ya juu. Sitazungumzia jinsi alivyoanza safari yake ya kuwa mwanamuziki. Ujio wake umeweka msisitizo kwenye kilio cha Fid Q.

One The Incredible. Courtesy: mxcarter.com

Binafsi nilidhani nyimbo zake mbili zitakuwa zinatikisa sana Bongo kuliko nyimbo za Mr Nice (enzi zile). Lakini nilipowauliza vijana wenzangu kwenye Jimbo la Mnyika, wengi walisema hawajawahi kuusikia wimbo unaoitwa “Pure Number.” Nimeusikia huu wimbo mara moja tu kwenye majuma mawili yaliyopita.


Sikuamini, kwasababu kwa mtazamo wangu, nafikiri ule ni moja ya nyimbo chache sana unaofanya watu wafikirie. Ukiacha punch-line delivery inayonikumbusha wimbo huu, nyimbo imeshiba metaphors ambazo itakulazimu uusikilize tena na tena na tena. Kijana One ni maarufu zaidi kwenye mtandao, kitu ambacho kitakufanya uanze kuhoji mambo lukuki.

Nisingependa kuendelea kulia. Nawashauri wasanii wa Hip Hop kujipanga na kuwa na umoja. Kinachotakiwa ni kuwa na chombo mbadala ambacho kitawawezesha kuwasilisha kazi zenu moja kwa moja kwa hadhira yenu. Mkongo mpya wa mtandao ndio unakaribia kukamilika. Kwahiyo baada ya miezi michache nadhani idadi ya Watanzania wanaotumia mtandao itaongezeka kwa kasi. Msisubiri mkongo ukamilike ndio muanze kujipanga; inatakiwa muwe tayari kabla ya huo mtandao mpya kuanza kufanya kazi.

Bila shaka hapo ndipo mtakapoweza kuwaumbua wale wanaoichezea fani; wabinafsi ambao hawaoni mbali. Majukwaa mnayoyatumia sasa hivi yataboreshwa, ila ushirikiano wenu ndio utakuwa injini.

Na kwa kumalizia nina ushauri kwa One, mmoja wa wasanii ambao ninaamini hata Fid Q huwa anasubiria nyimbo zake: mashabiki wako wanakufagilia kutokana na unachofanya sasa hivi — kutokukurupuka, mistari inayofanya watu wafikirie na kughani kwa ufasaha. Mabadiliko yatakuja kadri unavyozidi kukua na kukomaa kwenye fani; lakini ukiwa makini, mabadiliko haya yatakusaidia kukuboresha na sio kukudumaza au kukupotosha.

Nilikuwa nasita kuandika makala kuhusu dogo baada ya kusikia wimbo wake wa kwanza. Kwasababu wengi wamekuja, wakatikisa kwa wimbo mmoja, halafu wakatokomea kama wamefunikwa na mawimbi ya tsunami. Bahati nzuri ilikuwa sio ‘bahatisha ndulute.’

Ukipata muda, tazama video ya wimbo wake wa kwanza ‘The Incredible.’ Ni ishara tosha kwamba video kali sio lazima iwe imejaa mambo ya anasa; vijana hatuhitaji hayo sasa hivi.

Msomaji, uwe mshabiki wa Hip Hop au la, usisite kuacha maoni yako kuhusu jambo lolote kuhusu mweleko wa muziki Tanzania.

Previous ArticleNext Article
Steven was born and raised in Dar es Salaam, and moved to Germany for his studies. He graduated with a BSc. in Physics (Jacobs University Bremen), and then a MSc. in Engineering Physics (Technische Universität München). Steven is currently pursuing a PhD in Physics (growth of coatings/multilayers for next generation lithography reflective optics) in the Netherlands. He’s thinking about starting his own business in a few years; something high-tech related. At Vijana FM, Steven discusses issues critical to youths in Tanzania, music, sport and a host of other angles. He’s also helping Vijana FM with a Swahili translation project.

This post has 30 Comments

30
  1. Naweza kufanya uchambuzi wa kumuweka katika scale, kumlinganisha na MC katuni, Mwanafalsafa, Complex (R.IP) na Hasheem. Itabidi nipost separately.

    Ila nimependa ughani

    Yap, yeayah
    Ah, M-Lab (M-Lab is in the house)
    Moko, don’t touch it
    Yeah,
    Ahsante, Ah

    Beat kali haifai bila vocal
    Daily nakula dry, niko high kama popo
    Fanya worldwide sio ku try kama local
    Fake MC ukijikoki mi na squeeze kama fofo
    Ah,
    Verse baridi vaa koti
    Salamu kwa wanangu wote sina ripoti
    Bado mishemishe sapoti mwanangu opi
    Kila biti natoboa kama juisi ya kijoti
    Ni discipliner nawasimamisha wima
    Minya rapper [Mi nyarapa] mpaka sura kama simu ya kichina
    Mistari na vina, kwenye shari habari sina
    Mchagga halali, macho kwenye salari daima
    Zunguka kote hauna rafiki kama noti
    Sista duu hauna mnafiki kama shosti
    Tafuta deal uza hata pipi we bitoz
    Tafuta njia haya maisha hayamuliki kama tochi

    Chorus

    Chap chap chap chap ni sawa
    M-Lab, pure math, rap ni dawa
    Chap chap chap chap ni sawa
    Pure mathematics (dogo kapagawa)
    x2

    We unachana mi nachana mpaka basi
    Niko booth nina bic, karama na karatasi
    Sina hofu, nina speak salama kwa sala safi
    Ila ukinivaa vibaya nakuchana kama vazi
    Sanaa, gharama haramu chati
    Harakati hii kubwa hupaswi simama kati
    Verse inacheza Judo, kata na sarakasi
    Baba mama mbarikiwe kusimama kaa wazazi
    Pure namba, hapa zinajamba za kubuni
    Mshamba kawa mjanja, mjanja ana ujanja wa kihuni
    Banja kwenye beat weka ladha ya sabuni
    We ni base ten log mi ni namba ya kirumi
    Hii ni classic, hata isipotamba kama Dumi
    Kasi ya ma-rapper ina sanda kama uchumi
    Nina punchline na kick kama chuo kikuu cha ngumi
    Pure mathematics, sina banda n’na kampuni
    So

    Chorus

    Chap chap chap chap ni sawa
    M-Lab, pure math, rap ni dawa
    Chap chap chap chap ni sawa
    Pure mathematics (dogo kapagawa)
    x2

    Kuna rapper mwenye akili na rapper batili
    Rapper anayepata akisaka na asiyepata akisaka dili
    Tofauti kati ya rapper wa kwanza na rapper wa pili
    Wa pili anataka u-master huku hajapata umahiri
    Fungua ukurasa kwenye darasa la hip-hop
    Somo halisi tunaoandika kusikika anataka pomo
    Midomo inasikika ikisema na mikono
    Inashika makoleo na kuzika waliomo
    Waliopotea njia wanataka kurudi nyuma
    Wapotovu wamechuna, waovu wamenuna
    Inawauma,
    Wamepoteza mwelekeo,
    Maendeleo yamegota watafanya nini leo?
    Panapo matatizo tunataka suluhisho
    Likizo inawekwa kando tunakaza mpaka kifo
    Na tulivyo, sio watu wa matambiko
    Tumeshiteka kambi na kupekua maficho
    So,

    Chorus

    Chap chap chap chap ni sawa
    M-Lab, pure math, rap ni dawa
    Chap chap chap chap ni sawa
    Pure mathematics (dogo kapagawa)
    x2

  2. Naweza kuelewa kwa nini One hajapata “instant acclaim”. Anatumia
    metaphor zenye uzito ambao, mara nyingine zinaweza zisieleweke
    mara moja, katika utamaduni kama wa Nas.

    Naomfananisha na Hasheem (dogo mwingine mbaya sana sijui yuko
    wapi) au Complex (ametutoka mapema sana mkali huyu).
    Anapoanza anaeleza kwamba Hip-Hop ni zaidi ya beats, anatupa
    euphemism za ulimwengu wa hip-hop, anatuonyesha kwamba kuna
    haja ya kufanya kazi kimataifa, unapofikia mwisho wa ubeti wa kwanza, ushapata ushauri kwa kinadada kutowaamini sana rafiki zao wa
    karibu na kinakaka kujishughulisha kama wanavyosema waswahili
    “mgaagaa na upwa hali wali mkavu” na kukumbushwa kwamba maisha
    ni kutafuta, hakuna majibu yanayopatikana bila kutafutwa.

    Style yake ya ku deliver iko watertight, with the usual braggadoccio
    that is a hip-hop signature. Anaposema “we ni base ten log, mi ni
    namba ya Kirumi” namuelewa, yeye si rahisi kumuelewa na kumfanyia
    hesabu kama namba za kirumi, labda ndiyo sababu vijana
    hawajamtambua vizuri. Ma rapper wenye lyrical content yenye depth
    wanapata tatizo hili mara zote, kuanzia KRS-One mpaka Guru, labda
    ndiyo maana One amesema “Sanaa gharama, haramu chati”. Kufanya
    sanaa ya hali ya juu kunamgharimu msanii kwa kumfanya akose chati
    haramu ambayo angeweza kuipata kirahisi kwa kuimba vitu rahisi
    kuvielewa (wengine wanaita hii MC Katuni, Solo Thang kwa mfano kashasema hili). Na hili haliishii katika muziki tu, hata wasomaji wa
    tamthiliya za Dostoevsky watakwambia kwamba uzuri wake hautokani
    na wepesi wa kueleweka, bali ukifanya kazi ya kumuelewa na
    kumuelewa vizuri, ingawa itakuchukua kazi sana, lakini utafurahi na
    roho yako.

    Anapofungua ubeti wa tatu na kuongelea tofauti ya rapper mwenye akili na rapper batili, ni kama vile anatuambia kwamba hakimbilii u master kabla ya kupata umahiri. Na kama anataka ku perfect flow yake sijui ataanzia wapi maana anaonekana amejitosheleza, labda anaweza kujazia mistari mingi zaidi ambayo inapunchline zilizo accessible zaidi.

    Napenda imagery anayotoa akisema “Midomo inasikika ikisema, na mikono inashika makoleo na kuzika waliomo” ni kama anatoa challenge ya kutaka kuwazika ma MC wote wasio makini “waliopotea njia wanataka kurudi nyuma” . Nikimsikiliza na kusoma beti zake naona kama kuna kitu pekee ninachoweza kukisema kwa shaka ni kwamba naona kama ametafsiriwa kutoka Kiingereza moja kwa moja, na kama kazi zote zinazotafsiriwa kutoka lugha nyingine, kuna kitu kinapotea katika tafsiri. Ningefurahi zaidi angeweza kuwa na jinsi ya kutupata moja kwa moja kama Kibra, lakini bila ya kuyataja mavi mara nyingi kama afanyavyo Kibra. Inspector Harun katika nyimbo zake za mwanzo alikuwa ana uwezo wa kwenda verse nzima na maneno ya slang tupu (deep slang too) ambayo at the end of the verse yote yana tie in na ku make a tight delivery. Kwa hilo anahitaji kuongeza misamiati na vituko vya kiswahili, hususan uswahilini.

    Lakini pengine One si mtoto wa uswahilini na kumtegemea awe kama Kibra au kuwa na misamiati kama ya Inspector Harun si kumtendea haki, after all amesema mwenyewe yeye ni “Illmatic”, which takes something out of him kwa sababu tunajua Illmatic ni nani na One atakuwa mdoli tu wa Illmatic mwenyewe.

  3. Msangi, daaah!!…sijui nianze wapi…yaani jinsi ulivyoshuka na hii mimi mwenyewe hapa sina hamu mzee…heshima zako. Vipi, ulikuwa unapiga story na Incredible Uno mwenyewe nini kabla hujachangia..hah!!….safi sana mzee, nadhani na I hope kuwa uchambuzi wako utatoa changamoto kwa watu kufuatilia mambo na sio kusikiliza beat na chorus.

    Kwakweli baada ya kusoma uchambuzi wako, hata mimi nimeanza kuelewa kwanini huyu jamaa sio kipenzi cha wenye redio zao, kwani ili mtu kuweza kupata ulichokipata wewe, ni lazima msikilizaji uirudie rudie nyimbo au hata kutafuta mashairi yake.

    Mimi nadhani kuna umuhimu wa kumtafuta Uno mwenyewe, manake..dah!!….

    Huyu mshkaji sasa hivi yupo kwenye category ya peke yake, manake fasihi yake sio mchezo. Yaani kama rap zake ni somo, basi ni lile somo ambalo huwezi ukasoma dakika za lala salama alafu ukategemea kupasi mtihani, kwani huo mswaki wake utashangaa, lakini sasa marapa wengi bongo sasa hivi soundi nyingi.

    Nadhani pia delivery ya mshakji inavutia sana. Mimi am a fan, tangia nisikilize nyimbo yake ya kwanza.

    Complex simkumbuki sana, Hasheem ni balaa, tukizungumzia Mwana Fa sijui sasa tunamzungimzia wa enzi zile au wa sasa, na hilo linakwenda kwa Solo Thang pia.

    Uno mambo yako si mchezo mzee…na asante Mr. Msangi kwa uchambuzi ulio yakinifu.

  4. Itabidi nyimbo kama hizi zitumike kwenye somo la fasihi bongo, ili vijana waanze kuhakiki sanaa hii kama sanaa nyingine tulizosoma kwenye somo la Kiswahili O level. Kazi za akina, Fid Q, Hasheem, Mwana FA (early 2000s), Solo (early 2000s), Necha (early 2000s), Inspekta H (early 2000s).

    Hii sanaa acha, kuna watu wanaifanyia research, mfano Prof. Perullo huko Rhode Island. http://web.bryant.edu/~aperullo/publications.html

    Msangi nimeukubali uhakiki wako. ‘Nuff respek’. Unajua enzi zile za Inspekta watu tulikuwa wabishi kufuatilia lyrics, lakini wapi! Kama haujatokea mitaa ya TMK kuelewa mistari inakuwa shida – ila mbona walihit?

    ‘Uno’ inabidi aendelee na uzi huu huu. Ninasubiria track collabo ya huyu na ‘Stereo’. Yaani nyimbo moja, vesi kama 4 hivi peke yao, back-to-back – no chorus. Imagine hiyo track wakimuita Fid Q afanye opening ….

  5. Kwa bahati mbaya siwezi kusikiliza hiyo kopo kwa sababu ya internet zetu huku. Mp3 ndogo tu inachukua miaka. Na youtube wenye nchi yao wameiban.

    Anyways, ila niliisikia The Incredible kipindi fulani, ikabidi nivitafute vichwa vyangu vya bongo hip-hop kumjua huyu dogo. Kweli amejipanga.

    Kuhusu mtanange wa muziki wa Hip hop nyumbani,nakumbuka AY alikuwa anahojiwa, watu wakamuuliza kaka mbona siku hizi umebadilisha style mno? Ambwene akajibu kwamba wanaopenda Hip Hop hawaji kwenye concert wala hawanunui CD. Akasema kwamba kwake muziki ni maisha. Pia nadhani contrary to SN thesis, naona kwamba yule dada wa Clouds kwenye XXL pia yuko juu sana kuvipa airtime vichwa vya hip hop. I think Nick mbishi, and Nick wa pili wote wamepewa sana shavu na XXL.

    Kumalizia tu, kijana the Incredible anatisha, lakini kuna vichwa bongo ambavyo forever viko makini. Jay Mo, to me is hands down the best lyricist. Kama unaikumbuka Majukumu, you will know what I’m saying. Halafu huyu kijana anaitwa Roma Mkatoliki, yuko juu. “Walioacha tizi wakawa kama Mrisho Ngassa/Nakomba mapene yote kisha nasepa kama Lowassa” haa haa. JCB yupo juu, Nay wa Mitego is dope and the whole A-town hip hop scene is just dope.

  6. Dah, pole sana Selemani; labda utumiwe hizi nyimbo? Ili kupunguza machungu.. Dogo anaandika — kama wachangiaji hapo juu walivyosema.

    Nikki Mbishi, Joh Makini, Fid Q, N2N na wengine wanasikika. Lakini kuna mambo mengine zaidi yanapewa kipaumbele kwenye vituo vya redio. Najua kuna wapenzi wa aina nyingi za muziki, lakini hiyo haimaanishi kupiga nyimbo fulani mara 3-4 kwa siku, huku nyimbo nyingi ambazo ni nzuri zaidi zikiwekwa kapuni. Sasa hivi zimepita wiki tatu, na nimeusikia “Pure Namba” mara ile ile moja tu.

    Kuna mtazamo ambao labda utawahuzunisha watu wengi, kuwa watu wa Hip Hop hawaji kwenye concerts wala kununua kazi za wasanii. Tutamtafuta Fid Q mwenyewe ili atueleze album yake ya Propaganda inaendaje.

    Pili, watu ambao wanajua kuandika na kucheza maneno kama Uno, si huwa wanakatishwa tamaa na mambo kama haya? Mwishowe, kila msanii ana “dumb it down” na tunaishia kuwa na hizi nyimbo ambazo ni za wiki mbili tatu; hudumaza fikra na ile dhana ya muziki wa Hip Hop kuwa na chembe chembe za ushairi hatimaye kufa kabisa.

    Inasema nini kuhusu jamii yetu? Haya mambo yanajirudia kwenye kila mjadala nadhani…

    @ Msangi… Mwisho. Umenipa moto wa kuibua nyimbo zile za Uswazi. Ngoja, nikipata muda nitakuchokoza na my all-time favorite song: Hili Gemu (Sir Nature). Tutauchambua kila mstari mpaka tuulewe vizuri kwa kubadilishana mawazo. Maana’ke mpaka leo kuna mistari ambayo nadhani maana yake hubadilika, kutegemea nimeanzia wapi “kuunganisha” mistari au hadithi fulani.

    Yule Nature wa Nini Chanzo sijui kafia wapi.

    “Hela ya bia hatuna, si tunakunywa chang’aa
    Uzushi uzushi, mwanangu hatuzungushi…”

    Halafu KR anaanza:

    [Sijui] hana hela, halafu mtoto wa shangazi kutoka Vikindu katia timu ghetto; anaumwa anataka kupelekwa hospitali. Wakati hela ya msosi tu inampiga chenga ya mwili…

    Got carried away there, sorry!

    Anyways, tetesi za kuaminika: Hasheem “Dogo” yupo.. tuendelee kuombea kurejea kwake ulingoni!

  7. c unajua presenters ni warahisika ila kurahisika kwa urahisi hauendani na upembuzi na udadisi wa wetu ufanisi ila poa tu inabaki skendo ka padri kukimbia mazishi!!

  8. Msangi respect bro. Tunahitaji kufanya uchambuzi wa namna hii mara kwa mara sababu mwisho wa siku ni somo kwa mcs, djs na wadau wa muziki.

    Mara nyingi sana vijana hunifuata home kuniletea nyimbo ama niwape beats na pale nnapotaka niwape ushauri juu ya namna ya kutunga mashairi ya hiphop pamoja na jinsi kuflow vzr kwenye beats huwa nawasikilizisha zaidi ngoma ya One (The incredible). Hata kama nisiposema chochote wimbo wa mchz huwa ni somo tosha kwao. Wakazi aliwahi kusema kuwa alipoiskia the incredible aliamini sasa kumbe hiphop imerudi Bongo, which is true.

    Kwangu Pure number haikuwa my favorite pengine ni kwasababu sikuipa muda kuisikiliza kwa makini mwanzo hadi mwisho. Lakini kuna sababu ambazo zinaifanya trak yake The incredible ijulikane zaidi kuliko hiyo ya pili aliyotoa. The incredible is classic, beat nzuri na ule ubunifu wa scratches kwenye hook.

    Na pia ujue kuna nyimbo nyingine kuzielewa ni mpaka uumize kichwa kama msanii mwenywe alivyoumiza kichwa kuandika.

    Jos Mtambo alikuwa anahojiwa na Planet Bongo( Channel 5) akasema kuwa mashabiki wengi wa muziki hawapendi nyimbo ngumu kuzielewa, ndo maana kama alivyosema Msangi kuna haja pia ya waandishi mahiri kama akina One, kuchanganya pia lyrics ambazo hata washkaji wa mtaani wasiojua kitu kuhusu hiphop waelewe content ya wimbo. All in all One ni tafsiri yangu ya mapinduzi ya hiphop Tanzania. He is my favorite mc.

  9. Unayosema yana ukweli. Lakini sioni sababu ya msingi wasanii kuandika nyimbo rahisi ili tu kupata wasikilizaji/mashabiki wengi. Hoja yangu ni kama ifuatavyo:

    Wahusika kama kina One, Stereo, Fid Q, Nikki Mbishi wakiendelea kama wanavyofanya sasa hivi, basi Hip Hop itakua tu.

    1. Wasanii wengine itabidi wawe makini zaidi kwenye uandishi, kwasababu wanajua kila nyimbo itakayotoka itakuwa inalinganishwa na classics za hao nilowataja na wengineo kama wao.

    Nadhani mtakubaliana na mimi kuwa nyimbo ikitoka, lazima watu (wanaofuatilia Bongo Hip Hop) watakumbushia Ngangari, Hili Gemu, Bila Sanaa, Chemsha Bongo au Vina Utata. Mbona Hili Gemu ilikuwa ngumu — na bado watu hawaielewi! — lakini watu waliikubali? Sikumbuki kama kuna mtu yoyote au Juma Nature mwenyewe aliichambua…

    Uzuri ni kwamba, sasa hivi tuna nyimbo nyingine ambazo ni fasihi; ushairi, vipaji, maisha, siasa, vijana, elimu… Rafiki, Propaganda ndio zangu sasa hivi.

    2. Tusiseme kuwa mashabiki hatupendi vitu vigumu. Cheza Pure Namba mara mbili mfululizo halafu utaona kitakachotokea. Isizimwe tu kwasababu ni ngumu. Nyimbo kama ile inatakiwa kusikilizwa kwa makini zaidi ya mara moja.

    Pia, zinaweza zikafumbua watu macho kwa kuwataarifu kuwa kuna mafumbo mule ndani. Au zikachambuliwa.

    Mfano: Propaganda ni wimbo ambao unaweza ukaonekana ni wa kawaida tu. Lakini ukimuelewa Fid Q, unaweza ukaandamana kupinga mambo fulani kwenye jamii.

    Mi’ binafsi nimemuuliza Fid Q, kwanini hakutoa ule wimbo kabla ya Uchaguzi? Anayozungumza kwenye beti mbili ni UKWELI MTUPU, lakini yeye anaziita au anaita ushairi wake propaganda; ni paradox.

    Kwa kifupi, ametumia sanaa kuiambia jamii kuwa mnachoamini kutoka kwa viongozi wa siasa mengi hayana ukweli. (Uulize maswali ili iweje!) Yaani, tunaamini propaganda na kuuzika ukweli — ndio tulichochagua.

    Sidhani kama ni wazo la busara kumwambia “dumb down your flow”; bali tuwasaidie kuchambua ushairi wao…

    Kwa kumalizia tu, tutaendelea kuchambua nyimbo kama hizo ili kufumbua watu macho. Watakaosoma na wasome. Wiki ijayo: Propaganda!

  10. yeah, tatizo la media kutokuwapatia wananchi chakula ya ubongo i mean HIP HOP music ni kubwa tena kubwa zaidi ya stories. mimi binafsi naamini nina jukumu la kuhakikisha muziki huu unapata nafasi kadri ya uwezo wangu,tatizo ni ushirikiano kwa hao wasanii wenyewe… wameshakata tamaa baada ya kuona wanabaniwa so hata hawaangalii njia mbadala ya kutatua tatizo, wachache wameweeza simama but wengi wako shimoni japokuwa wanaandika mistari iliyoshiba faida, wajaribu kutumia media mbadala including websites kama hizi and even mine ujazo.com ili waweze kujitangaza sio wanakaa doro mpaka watafutwe wao.

    as for my fellow radio or media people… nadhani umefika wakati ukweli upewe nafasi yake zaidi ya maslahi na matakwa ya nafsi…TOP…UJAZOOO!!!

  11. Si mchezo, hili suala la kutaka wasanii wa-dumb it down ni mfano mzuri wa huu mstari kutoka kwenye Propaganda “tunajenga tabia kisha tabia zinatujenga”, sasa inabidi tufanye reverse psychology. Yaani, ni kukazia hayo hayo mashairi ya kina, na hao wanaosema kuwa hawataki mashairi magumu watabaki kuwa hawana option bali kusikiliza na kubadili tabia walioijenga, na kuacha tabia ya kukubali tabia ya kupenda nyimbo zenye mashairi yasiyo mepesi kuwajenga wao…

    Hii imenikumbusha nyimbi hii ya Lupe: http://www.youtube.com/watch?v=q1Et1siZhTk&ob=av2el

  12. ..kwa mimi binafsi one namchukulia incredible kama alivyojinadi, kwenye simu yangu nina nyimbo zaidi ya 300 ila kwa siku uwa nasikiliza nyimbo huyu jamaa mara nyingi za ya zote.

    Cha ajabu ni kwamba kila nyimbo anayoitoa uwa naielewa na kuipenda mara moja tu ninapoisikiliza.
    Hata uandishi na upangiliaji wake wa mashairi uko poa, ingawa ni mgumu kumuelewa kama hauko deep sana kwenye hip hop, hata yeye nafikiri kaliona hilo, na ndio maana mwisho wa verse ya kwanza ktk wimbo wa THE INCREDIBLE, amemaliza namna hii

    “TUNGO KWA CHAPTER, UMEPATA NINI HAPA?”

  13. One ni mkali ukijumlisha na vichwa vingine pale M lab unakutana na ukali usio kifani.

    Jana nilihudhuria uzinduzi wa Mixtape yao inayokwenda kwa jina la The Element, naweza kusema ilikua ni show ya hali ya juu sana, maana kama miujiza akina Zavara, Sameer X wa Kwanza Unit walipanda kwenye stage. Prof J alikamua verse zake za kiingereza kiukweli ilikua ni Side B ya Prof ambayo sikuwahi kuishuhudia hapo kale. Fid Q alibamba sana pia kwa upande wake.

    Wasanii wengine kama Mansu Li na JCB pia walifanya vyema. Lakini juu ya yote, One, Stereo, na Nikki Mbishi waliangusha vitu ambavyo kiukweli kila mtu alihamasika na kufarijika kwamba Hip Hop imerudi kwa kiwango cha hali ya juu

    Big Up kwa mkuu Duke Tachez hakika usiku ule ulikua ni wa mafanikio makubwa na watu watakumbuka hata ukamilifu wa dahari. Tunasubiria next mix tape.

    The Solon.

  14. Msangi,U rock big timez man,dah yaani kuna sehemu ambazo sikuwa nazielewa kiukweli ktk pure namba lkn umesaidia saana,mimi binafsi najivunia sana nchini mwetu kwa sasa kuwa na mwanahiphop One,pia nimependa baada ya kuchek interview yake alipoulizwa wasanii waliomu-influance kuingia kwenye game mmoja wapo ni hasheem(dogo),nafarijika sana,Msangi,man nahitaji sana ku contact na wewe kama inawezekana,mail yangu jzaggy@hotmail.com
    kwa kumalizia tu niwatakie mafanikio mema katika shughuli zenu za kila siku wachangiaji wenzangu(msangi,bahati,joji,selemani,SN,skywalker na wengineo)…mungu ibariki tanzania,chadema na dr slaa.

  15. Me cna lakusema juu ya one cz jamaa yuko deep japo apewi air time yakotosha inauma kuona vchwa km one, salu t, vnataka kupotezwa kwenye raman ya hp hop kwakuvnjwa moyo na media hapa bongo namkubal sana one nando mc pekee alye nfanya nwe hp hop rapa like him. Nakujua kumekja afta kuchana nymbo zake bila utata. Bg up kaka kwa makala hii

  16. sina mengi ya kusema One yhe incredible for the first time namsikilaza kwa redio nilishangaa sana nikapata hamu ya kumjua huyu jamaa…hamu yangu ya kumfahamu bado ilizidi siku nilipokuwa na Nikki,pamoja na TEXAS alikuja tukawa naye tunapiga story wote maeneo ya Morocco lakini sikuweza kumfahamu kama ndo yeye kwa wakati ule….eeh bwana eeh kilichonistua ni pale Nikki alipomuita “ONE njoo kwanza” ilibidi nifunguke kwa kumuuliza NIKKI huyu do the incredible.

    tHE INCREDIBLE NI NOUMER SANA,MSANGI KASHAMALIZA YOTE BAAAAAAAAAAAAS

  17. Kusema kweli ONE ni MC shupavu kwa hapa bongo. Toka mara ya kwanza naisikia incredible nilivutiwa na the way anavyoimba na matamshi yake ya maneno lakini kikubwa zaidi ni mistari yenye vina na yenye maana. Kwa mtu wa kawaida itamchukua dakika kadhaa kumuelewa anazungumzia nini but for me it takes seconds kumuelewa and i really enjoy listening to his songs hasa pure namba haipiti siku sijaipiga hiyo nyimbo.

    nick mbishi yupo vizuri nae napenda track yake kaimba na grace matata ile nyakati za mashaka. nina albam yake sauti ya jogoo kama hujapata kuisikia nunua copy yako usikie kijana kakaza.Stereo nae yupo safi sana tuu, katika albam ya nick mbishi kuna nyimbo wameimba stereo, one na nick mbishi mwenyewe. Sikilizeni ile nyimbo.

    Ujumbe wangu kwa watanzania wote hasa tunaopenda hip hop, tuwape sana ushirikiano wasanii hawa wa hip hop coz wanaelimisha sana jamii wanaimba vitu vya maana sana kwa mtu makini. nimejaliwa uwezo wa kusikiliza na kuelewa haraka hip hop ndo maana naipenda.

    ONE me nasubiri kusikia zaidi na zaidi. popote pale nikisikia sauti ya one lazima nitasimama nijiulize ni nyimbo gani na ntapenda kusikiliza anachokiimba coz huwa kina maana siku zote.

  18. one we ni future ya hiphop in Tz now! Kaka kwanza unajua kuandia na hukurupuki pia unaonyesha unaumiza kichwa. Kaza ileile kaka tamaa ya pesa isije ikaaribu mziki wako. Tuliongelea hiphop kila kitu kipo kwako:. Nilicheki pia freestyl zako cheusidawa tv mia unatisha londuno for life mnajua.

  19. daima ukweli utabaki ukweli na uongo utasadikika,kama kuna m2 amesikiliza nyimbo za one the incredible na kuzielewa basi huna haja ya kumuuliza huyu mshkaji ni noma,na binafsi naamini real hip hop haiko redion bali kitaa kinaujua ukweli,na kama kungekuwa na uwezo wa kuanzisha media ya hip hop only basi ingekuwa fresh,mimi binafsi baada ya kutambua ukweli kati ya hip hop na media za kibongo wanazibagua ladha hizo wamenifanya nianze kuzichukia media hizo cause nikisikiliza hp kuna something na gain kwa brain yangu,lakini one day yes wadau au vp?

  20. eeeee bana no one like one he knows de clasic music big up.kwa bongo hii wapo wawili 2 ye na brodah FID Q

  21. Ebwana dah! me nasema kuwa UNO hana mpinzani hapa TZ, Siku ya kwanza tu niliyomsikia katika radio nikajiuliza huyo ni nani na wimbo ulipoisha nikataka niurudie tena na tena lakini kwa bahati mbaya nikakumbuka kuwa wimbo ule ulikuwa unachezwa kupitia kituo fulani cha radio na siyo katika moja ya CD zagu za nyimbo.
    Baadhi ya wasanii bongo ni wababaishaji, coz utakuta mtu anatunga wimbo asubuhi then jioni yupo studio anarecord. lakini angalia nyimbo za huyu jamaa sio nyimbo za kukurupuka hata kidogo ndo maana anakwambia verse zake zinacheza judo, kata na sarakasi. pia madj na ma presenter wetu wanatabia ya kutuchezea nyimbo za watu fulani tu kila siku lakini nyimbo za watunzi wanaotumia akiri zao vizuri zinaachwa.
    Huyu jamaa anapenda aitwe pure number lakini me ningependa kumuita the genius. mpo wachache sana hapa TZ kama niki mbishi, sterio na Farrid kubanda. Big up sana brother.

  22. ebana one we ni moko wa miujiza nimekubali ni zaidi marap,nakosa ujasiri yaani nakosa cha kusema we ni mtu wa aina gani kwenye huu mziki wa HIP HOP kiukweli wengine watasubiri sana coz unayoyafanya ni miujiza.

  23. Sio siri UNO amejipanga ajavamia gem namkubali sana uyu bro.ila ni media tu ndo zinabana ila ipo siku zitaachia.so kuna kituo kimoja cha radio uku mbeya nakipongeza kunakipindi cha mchana kinaitwa hotty show huwa atakama sijaingia mtandaon napata kuskiliza nyimbo nyingi za hiphop mya na za zaman kupitia hi radio niliwatambua wasanii kama Mwanahapa,kadgo,songa na wengine wengi.one day hip hop itakubalika bongo japo ni wachache tunao ikubali na kuipenda I m hip hop forever.

  24. One z ma favorite… ukickiliza mtanganjia,haya mausha,salam,hzo mlzoztaja,got em,debut, cold,wasumbufu wa kizazi,you wont win,understanding the struggle… na nyingne .. one kweli he is a pure number … hamna hata moja kata ya nymbo zakr nkakosa kitu… hata akishrkishwa … kwanza he understands nin anafanya na akifanya kweli anafanya. … hiphop imkua sasa …..

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Send this to a friend