Vyuo vikuu niaje?

na Sakura

Wakati tukiendelea kutafakari elimu inayotolewa kwenye shule zetu za sekondari, mimi natupia jicho vyuo vikuu vyetu. Je, wanafunzi wanatumiaje fursa wanazozipata wakiwa vyuoni?

Kumekuwa na mijadala kadhaa kila kona inayozungumzia na kujadili nafasi ya wanafunzi wa vyuo vikuu katika kuanzisha biashara na makampuni. Kama mnavyojua, makampuni mengi mashuhuri ulimwenguni yalianzishwa kwenye mabweni vyuoni kupitia ubunifu binafsi wa wanafunzi (Facebook, Google, Time Magazine, Tripod.com, FedEx).

"Vitabu Madesa"

Sawa, tunakubali kuwa ni vigumu kuanzisha biashara ya mtaji mdogo ikastawi katika jamii yenye uchumi mbovu  — zipo tafiti zinazoonesha kuna fursa za biashara zaidi katika nchi zinazoendelea kuliko zile zilizoendelea — lakini tukumbuke kuwa hata hizo fursa chache za wazi zilizopo hatuzitumii. Ningetarajia kuona kampuni ya uuzaji vitabu vilivyotumika  — kwa mfano, www.vitabu-madesa.com — ikifanya kazi vyuoni mwetu kwa kuwa soko la uhakika lipo.

Hatuoni hilo, badala yake tunakutana na migomo kila siku. Nisingependa kuingilia siasa hizi za migomo, lakini najiuliza, hivi kwa nini hakuna anayejaribu kufanya kazi za muda au vibarua ili kujikimu walau kidogo? Kweli, wanafunzi wa fani ya uhandisi hawana muda wala nafasi ya kufanya kazi wakati wa muhula wa masomo; lakini siamini kuwa wanafunzi wa masomo mengine hawana nafasi ya kufanya kazi mwishoni mwa wiki.

Hatusemi wala hatutaki vijana wa vyuo vikuu kushughulika zaidi na kazi za kujiongezea kipato mpaka kufikia kufanya vibaya kwenye masomo yao, lakini hakuna ubaya wa kuiga mtindo wa maisha wa wanafunzi wa ughaibuni pale inapolazimu, ambapo takribani zaidi ya nusu ya wanafunzi hususan wale wenye madeni ya mikopo hufanya kazi za muda wakati wa muhula wa masomo.

Makala nyingine:

Previous ArticleNext Article
Steven was born and raised in Dar es Salaam, and moved to Germany for his studies. He graduated with a BSc. in Physics (Jacobs University Bremen), and then a MSc. in Engineering Physics (Technische Universität München). Steven is currently pursuing a PhD in Physics (growth of coatings/multilayers for next generation lithography reflective optics) in the Netherlands. He’s thinking about starting his own business in a few years; something high-tech related. At Vijana FM, Steven discusses issues critical to youths in Tanzania, music, sport and a host of other angles. He’s also helping Vijana FM with a Swahili translation project.

This post has 8 Comments

8
  1. Elimu ya Tanzania imekuwa ya kubahatisha, mfumo mbaya wa kutarajia ajira kwa serikali, no practicals, tunafanya theory bwana. so ngoja tu crame mpaka tupate bachelor zetu.

  2. Wakati mwengine tunalaumu mitaala wakati tuna fursa za wazi tunashindwa kuzitumia. Au ndo tuseme mfumo wetu haufundishi ‘ushidani’ na ‘kujitegemea’?

    And I thought the CCM mantra is Ujamaa na kujitegemea!

  3. Swali zuri sana na miye nimekuwa nikijiuliza hivyo hivyo kwa muda sasa. Kabla sijaanza naomba nikusahihishe kidogo, hakuna taaluma rahisi au ngumu kuliko nyingine; ugumu na urahisi unakuja na malengo ya yule anayejifunza taaluma hiyo.

    Mimi ni designer by profession, nilivyokuwa chuoni (nilivyoanza sasa kuingia katika masomo ya digrii yangu, yaani college of design) katika semester moja nikawa na madarasa matatu kila moja mara moja kwa wiki kwa saa tatu. Na kila moja minimum requirement ni saa 20-30 nje ya darasa (kutokana na nature ya real world and real-world simulated assignments) Hiyo ni practical tu (kwa kila darasa). Sasa kwa designer wewe mwenyewe inabidi ujisomee zaidi ili ku compete maana hizi ni portfolio classes. Inabidi ujisomee mwenyewe ziada ya vitu kama design theory and criticism, constant visual and historical research, semiotics, Art History ya ulimwengu, Design history na kwa mimi mgeni bado kuna kuendelea kujifunza culture isiyo yangu kwani mimi sikukulia huko nilikokuwa. Ukiwa na bahati sana unalala saa 5 kwa siku sio zaidi ya hizo. Kwa hiyo sidhani kuwa kuna yeyote mwenye ahueni labda ana tatizo la kupanga muda wake vizuri zaidi.

    Ila ninachoweza kusema ni bado wanafunzi wengi fikra za kusomea mitihani ili kufaulu na hatimaye kuajiriwa; hatusomei kuelimika ili kujitegemea. Hii tabia inakuwa compounded na kulazimika kutumia second language (au third) katika kujifunza huko vyuoni.

    Kuanzisha kumpuni ndogo ndogo au kufanya kazi part time ni sehemu ya kujifunza jinsi ya kujitegemea na hususan “problem solving”.

    Vyuoni ni mahali bora zaidi na pengine hata rahisi kufanya hivyo kwani unakuwa pool ya watu wengi ambao mnaweza kushirikiana kimawazo na hata kivitendo pale mnapofikia kuanzisha huo mradi. Kuna support system kubwa na vilevile waalimu na wataalamu katika fani zao ambao wanaweza kuwa washauri wenu katika hiyo miradi.

    Elimu ni chombo tu cha kujijengea maisha bora kwako binafsi, taifa lako na hatimaye kwa binaadam wote.
    Kufaulu darasani kwa kuwa bingwa wa kukariri ni kufeli kimaisha na madhara yake tunayaona sasa hivi huku makazini–watu wamepasi vizuri lakini akipata changamoto katika kazi yake anashindwa kufikiri na kupata utatuzi. Kufikiri kunakuja kwa kufanya mazoezi ya kuchanganua vitu na situations tofauti na fursa pekee ya kupata hizo nafasi ni kwa practice ili uweze kukumbana nazo tu hakuna njia nyingine.

    Labda niulize wenzangu hivi vyuo vikuu vyetu viko serious kiasi gani katika kushirikiana na makampuni ili kutengeneza mazingira ya kuwawezesha wanafunzi kufanya internships au part time jobs?

  4. @Mkuki, Nakubali kuwa hakuna masomo mepesi na masomo magumu lakini pia sidhani kama ni haki kumtegemea medical student kwenda kazini physically during school term na ni hivyo pia kwa fani nyengine nyingi.

    Mimi nimesoma Architecture and Building Construction which requires hayo yote uliyoyataja pamoja na kuhakikisha naelewa masomo yangu ya engineering kama structural design, earthquake engineering, materials dynamics, ….. Nilikuwa literally naishi lab.

    Juu ya hivyo ilinipa fursa ya kujuana na watu kutoka mataifa mbali mbali na kuweza kutumia hiyo network pamoja na rafiki yangu aliyekuwa akisoma finance (alionekana na muda zaidi yangu) kuanzisha uwakala wa freelance translators kwa television networks kwa sababu niliwahi kufanya kazi part time kwenye network moja wakati wa likizo.

    Kwa hiyo kama ulivyosema, ni suala la kujipangia muda wako vizuri pamoja na kuangalia resources ulizonazo tu na wala si kitu cha kusema unasubiri mitaala ya shule ikufunze. Pia hakuna ubaya wa kufanya kazi za muda kwenye sehemu ambazo hazihusiani na masomo yako, experience unayopata pale unaweza kuja kuiingiza kwenye profession yako baadae.

    Suala la kusubiri serikali ituwekee mazingira mazuri ya masomo tusahau, wanafunzi wenyewe wachukue hatua kwa wanachoweza kufanya. Wanaweza kuanzisha clubs ambazo watazitumia kushiriki kwenye inter-university na international projects competitions kwa kuanzia ambayo itakuza uwezo wao wa kushindana na deadline pamoja na kunyanyua viwango vya kazi zao.

    Kupitia hizi clubs pia wanaweza kualika wataalamu kuwafunza namna ya kuandaa mikataba, kusimamia kampuni kama hayatolewi mafunzo hayo darasani.

    I hope vyuo vikuu vyetu vinatoa fursa kwa wanafunzi kuchukua units za masomo yasioingiliana na fani zao moja kwa moja. Department moja kwa nyengine.

  5. @Sakura nimekuelewa, na nafurahia mapendekezo yako hususani kuanzisha inter-university projects.

    Ulimwengu wa sasa unataka watu wanaojua ku synthesize fani tofauti kwani projects nyingi sasa zinahitaji interdisciplinary capacity ili kuzifanya ipasavyo inachohuzunisha ni kuwa wanafunzi wengi bado hawaelewi hilo na pengine mazingira ya vyuoni haya encourage wanafunzi kushirikiana baina ya fani mbalimbali.

    Ndio maana inakuwa ngumu kupata homegrown solutions maana hakuna watu wengi wanaokuna vichwa kutafuta opportunities.

    Lakini je ni kosa la wanafunzi au mfumo wetu wa elimu ambao umeshindwa kufuata mahitaji ya mwanafunzi wa leo? Je jinsi tunavyolelewa tangu tukiwa wadogo huwa tunahimizwa kujaribu vitu vipya? Je mfumo mzima wa malezi umesukwa ili kumfanya mtoto awe ni wa kupokea tu maelekezo au wa kuhimiza udadisi? Pengine kutoona opportunities sio ishara ya uzembe wakati mwingine inaweza kuwa hukufundishwa kufumbua macho. Pengine haya maswala ya elimu inabidi pia tuanze kuyaangalia kwenye kioo tuone ni jinsi gani sisi kama jamii tunahusika na kuzorota kwa shule na mfumo mzima wa elimu yetu.

  6. Mimi labda ningeomba swali langu liwe moja. Je, tunalionaje suala la kujitolea kwa watu wenye taaluma zao, na wenye mawazo mapya, tofauti, kwenda kusaidia mashuleni. Kwa mfano, mtu mmoja ua kadhaa wakapewa hata nusu saa pamoja na wanafunzi wa sekondari katika shule fulani kujadiliana nao haya masuala. Je, hii si itawapa changamoto mpya, manake walimu tayari wana kazi kubwa ya kumaliza syllabus ili wanafunzi wajibu hiyo mitihani hayo…ni mtazamo tu

  7. Mkuki umehoji vitu ambavyo majibu magumu kidogo.

    Wazazi bongo hawana nafasi ya kulea. Watoto wanasoma bording schools wanaonana nao wakati wa vacations tu. Wanaosoma shule za kawaida pia, wanatoka asubuhi wanarudi usiku.

    Kwa hiyo kama mfumo huko shuleni ni mbovu, wazazi hawawezi kurekebisha kwa kiwango kikubwa.

    Labda tufanye kama alivyosema Bahati, tuanze kuvolunteer kufundisha vitu hivi kwa wanafunzi.
    Tatizo hapo ni wangapi wako tayari kuvolunteer? Jibu linaweza kutukatisha tamaa.

  8. Kama watu walikuwa tayari kulinda sungusungu kipindi kile cha Mrema, nadhani ni kitu ambacho kinawezekana kukiwa na mpango kama ule wa sungusungu, the only thing different this time, sungusungu watakuwa wanalinda elimu ndani ya madarasa.

    Pamoja si mshabiki wa mfumo wa elimu na plan za elimu za Sirikali hii, lakini nadhani kama ni kulaumiana, kwa kiasi fulani tunabidi tugawiane, although Sirikali inazidi kukatisha watu tamaa.

    Nadhani Sirikali inabidi iwe mfano mzuri ili i-motivate watu kufanya kitu ninachoki-suggest. Wazazi wanaopenda kupeleka watoto zao boarding school hasa watoto wadogo, ni wazazi ambao wanakimbia responsibilities zao; mtazamo wangu tu. Huwezi ukategemea watoto wako walelewe na mtu mwingine, alafu baadae ukasirike unapoona mtoto wako anatabia mbaya na wala hajifunzi kitu chochote.

    But all in all, Sirikali ina mengi ya kufanya, kwani mpaka sasa hivi takwimu zinasikitisha…

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Send this to a friend