Bila Sanaa

Mimi kijana,
Bila Sanaa, ningeonekana mjinga,
Nisiye na fedha mimi,
Lakini sasa namshukuru Mungu mi’ najulikana,
Na mkwanja nakamata ile kisana.
Mimi kijana, ningeonekana sina akili.

– Imam Abbas & Juma Nature

Kuna vijana ambao huchukulia muziki kama sanaa; hukaa chini, huangalia jamii, wakajiangalia wao wenyewe, kisha wakaandika mashairi na kutengeneza tungo ambazo zitagusa na kuamsha fikra za watu wengi.

Nyimbo kama hizi — hasa zenye mafumbo au lugha ya ushairi — huhitaji kusikilizwa mara kwa mara. Hivyo tumeamua kutengeneza orodha ya tungo makini; playlist hiyo inaitwa “Bila Sanaa” , itakuwa mojawapo ya Projects zetu.

Huu ni mwanzo tu. Tutakuwa tunajaribu kuongeza nyimbo za zamani na mpya ambazo zinarandana na zilizopo — yaani, zinazogusa mambo tunayojadili kwenye tovuti yetu na changamoto kwenye jamii yetu, hasa kwa upande wa vijana.

Tafadhali, tusaidiane kufikisha ujumbe huu!

Previous ArticleNext Article
Steven was born and raised in Dar es Salaam, and moved to Germany for his studies. He graduated with a BSc. in Physics (Jacobs University Bremen), and then a MSc. in Engineering Physics (Technische Universität München). Steven is currently pursuing a PhD in Physics (growth of coatings/multilayers for next generation lithography reflective optics) in the Netherlands. He’s thinking about starting his own business in a few years; something high-tech related. At Vijana FM, Steven discusses issues critical to youths in Tanzania, music, sport and a host of other angles. He’s also helping Vijana FM with a Swahili translation project.

This post has 4 Comments

4
  1. 1. Tumeamua kuipa hii playlist jina “Bila Sanaa” kama shukrani kwa Bahati aliyekuja na wazo hili. Jamaa anaupenda wimbo “Bila Sanaa” wa Imam Abbas kupita kiasi!

    Hivyo basi, huo wimbo utabaki kuwa kwenye playlist muda wote.

    2. Wimbo No. 41 ni wa Kikosi Cha Mizinga. Nimefanya makusudi kuuweka ule wimbo kwenye namba hii maalumu kwa wakazi na mashabiki wa “Block 41 Kinondoni”.

    Sijui kama jamaa wangenitafuta na kunipiga makonzi kama ningeweka wimbo mwingine pale… maana’ke tunawaelewa wale masela kwa kutembeza mkong’oto!

    Enjoy!

  2. AWK, Bongo Flava ipo na “mzuka wake bado upo”. Ila, nadhani itabidi uwatakie radhi baadhi ya wasanii ambao nyimbo zao zipo kwenye playlist. Hasa yule “No. 53″…

    Pia, tunapenda kumshukuru Fid Q kwa kutupa ruhusa ya kuweka nyimbo zake mbili ambazo hazijatoka kama single i.e. Mwanamalundi na Hey Lord.

    Bila kumsahau Michael Mx Mlingwa kwa mchango wake!!

    Kama umezipenda nyimbo kutoka kwa One (The Incredible, Pure Namba), Nikki Mbishi + Suma (Hisia, Punch Lines) na Stereo (Rafiki + New Era Muzik), tafadhali nunua mixtape yao hapa: The Element Mixtape. Kuna nyimbo nyingine ambazo ni nzuri; kama “Nitabaki” na “Karibu”… unaweza ukapata preview.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Send this to a friend